Ukristo hatarini kupotea Iraq

IRBIL, IRAQ

Askofu mkuu wa Irbil, mji mkuu wa jimbo la Iraq la Kurdistan, amewashutumu viongozi wa kikristo wa Uingereza kwa kushindwa kufanya juhudi za kutosha kuilinda jamii ya inayotoweka ya Wakristo wa Iraq.Katika hotuba aliyoitoa mjini London jana, Askofu huyo, Bashar Warda alisema kuwa Wakristo wa Iraq sasa wanakabiliwa na hatari ya kutoweka baada ya miaka 1,400 ya kuuawa.

“Tangu majeshi ya Marekani yalipovamia Iraq na kuuondoa madarakani utawala wa Saddam Hussein mnamo mwaka 2003, jamii ya Wakristo imepungua kwa asilimia 83, kutoka watu milioni 1.5 hadi watu 250,000.

“Ukristo nchini Iraq, ambao ni moja ya makanisa ya kale, kama si ya kale zaidi duniani, unakaribia kutoweka. Wengine wetu tuliobakia lazima tuwe tayari kukabiliana na kufia dini ,” alisema.Alikuwa akizungumzia tisho kubwa la hivi karibuni kutoka kwa wapiganaji wa jihadi wa Islamic State (IS) kuwa ni “vita vya mwisho vya Wakristo”, kufuatia mashambulizi ya awali ya kundi hilo mwaka 2014 yaliyowasambaratisha wakristo 125,000 kutoka makazi yao asilia.

“Wanaotutesa wanamaliza uwepo wetu, huku wakitaka kupangusa historia yetu na kuangamiza maisha yetu yajayo,” alisema askofu huyo.

Aliema nchini Iraq hakuna fidia kwa wale waliopoteza mali zao, nyumba wala biashara, huku maelfu ya Wakristo wakiwa hawana la kuonyesha kuhusu maisha yao ya kazi, katika maeneo ambapo familia zao zimeishi, labda kwa miaka elfu moja.

Islamic State wanaofahamika katika ulimwengu wa kiarabu kama Daesh, walifukuzwa kutoka ngome yao ya mwisho ya Baghuz nchini Syria mwezi Machi baada ya kushambuliwa na wanajeshi wengi wa mataifa mbali mbali na kusema kuwa ulikuwa ndio misho wa “mtawala wa kiislamu”.

No comments