Mapadri kuruhusiwa kuoa "Vatican "


Vatican City :
 Makao makuu ya kanisa katoliki duniani Vatican, yamefungua rasmi mdahalo juu ya suala la kuruhusu wanaume walioowa kutumikia kanisa kama mapadri katika maeneo ya vijijini ya Amazon ambako mapadri ni wachache.

Wito wa kufanyika madahalo kuhusu pendekezo hilo ulitolewa katika waraka wa kanisa uliyochapishwa kuelekea mkutano wa maaskofu wa Amerika ya Kusini kutoka eneo la Amazon utakaofanyika Oktoba mwaka huu.



Katika waraka huo wa kanisa imependekezwa kuwe na uwezekano wa kutawazwa kuwa mapadri wazee wenye umri mkubwa na hususan wazawa na wanaoheshimika na kukubalika na jamii zao hata ikiwa wameoa.
          

No comments