Askofu Wafula afungua kanisa jipya huko Mombasa
Askofu Robert Wafula ambaye alikuwa akihudumu katika kanisa la Neno Evangelism tawi la Mombasa amefungua kanisa lake wiki chache tu baada ya kuondoka katika kanisa lake James Maina Ng'ang'a katika njia ya kutatanisha
Aliandika katika ukurasa wake wa FB hivi
Ningependa kuwakaribisha katika ibada ya maombi Jumanne hii katika ukumbi wa Mombasa Women Hall kuanzia saa kumi na moja unusu jioni. Hatutafanya ibada mahala hapo kwa heshima yake mchungaji wetu James Maina, kwani hapo ni mahali pa wafuasi wake kuabudu. Mungu awabariki na karibuni Mombasa," alisema.
Ujumbe wake uliwavutia waumini wake na Wakenya wengine ambao walimtakia kila la heri wakati akianza wito wake mpya.
Wafula amefungua kanisa lake majuma machache baada ya kulitema hadharani kanisa la pasta Ng'ang'a la Neno Evangelism baada ya kushambuliwa kwa matusi.
Chanzo:Tuko
Post a Comment