Msabato akataa kuzika udongo wa familia yake iliyokufa kwenye ajari ya ndege
Raia wa Kenya aliyewapoteza ndugu watano katika ajali ya ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia amekataa kuzika udongo uliokusanywa kutoka katika eneo la ajali.
Paul Njoroge amepoteza mke,mtoto wa kike,na wajuu watatu ambao walikuwa abiria katika ndege ya Boeng 737 Max-8 iliyoanguka jumapili ya Machi 10 na kuua abiria 149 na wafanyakazi wanane.
Jumatano Machi 20 mwaka huu katika huduma ya maombi iliyofanyika huko Bahati ,Nakuru,Njoroge ambaye ni Mwadventista wa Sabato amesema amepokea kwa maumivu na masikitiko tukio laa kuondokewa na ndugu na kwa sasa anasubiri matokeo ya vipimo vya vinasaba (DNA) japo muda uliotolewa ni mrefu .
Ameeleza kuwa kipindi cha miezi sita kilichotolewa na serikali kwa ajili ya kufanya upembuzi wa vipimo vya vinasaba kutoka katika vipande 5000 vya mabaki ya miili iliyokusanywa kutoka katika eneo la ajali ni kipindi kirefu hivyo atafarijika tu kwa huduma ya maombi ya faraja kwa ndugu na jamaa ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo ambayo itafanyika Machi 29 mwaka nchini humo.
Njoroge ambaye amepoteza ndugu hao watano amesema imani ya dini yake hairuhusu kuzika udongo uliokusanywa kutoka Bishoftu kilomita 60 kusini mwa mji wa Addis Ababa ambako mamlaka zinafanya uchunguzi wa kutambua miili ya waliopoteza maisha.
“Hili ni jambo kubwa kwangu,linaumiza sana,lakini nafikiri hakuna ninachoweza kufanya bali kulipokea na kulikubali na acha watu waendelee na maisha”amesema Njoroge.
Shirika la ndege la Ethiopia limesema litalipa fidia kwa familia zilizopoteza wapenda wao kutokana na ajali hiyo ya ndege.
Post a Comment