Uraia wa Askofu Kakobe kuleta utata!
Taarifa zilizotoka jioni ya April 7 2018 zimeeleza kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Idara ya Uhamiaji imemuandikia barua Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Zakaria Kakobe kumtaka afike katika ofisi za Idara hiyo kwa ajili ya mahojiano.
Askofu Kakobe anatakiwa kufika katika ofisi hizo siku ya Jumatatu Aprili 9 saa 4 asubuhi na kuonana na Afisa Uhamiaji wa Mkoa ili kuhojiwa kuhusu uraia wake ambapo tayari Askofu Kakobe amethibitisha kupokea wito huo na amesema yupo tayari kwenda.
Baada ya watu mbalimbali kutoa maoni yao juu ya kuitwa kwa Askofu Kakobe, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole alichukua muda wake kuandika yafuatayo >>> “Mbona kuhojiwa jambo la kawaida? baadhi ya watu wanajenga tabia ya hovyo sana”
“Watu “wakubwa” wakiitwa kuhojiwa inaonekana kitu cha ajabu. Mbona huku mtaani kuhojiwa Polisi ni kitu cha kawaida tu, tuanze kuzoea na hasa ktk awamu ya 5 kwamba, na tunasisitiza binadamu wote ni sawa” – alimalizia kwa kuandika Humphrey Polepole

Post a Comment