Mwambe(Mbunge wa Ndanda) ataka makanisa kuponya Ukimwi

DODOMA-TANZANIA. Mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe ameomba taarifa bungeni akihoji kama kanisa la Mlima wa Moto la mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk Getrude Rwakatare linatoa maombi ya kuwaombea na kuwaponya wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi ili kuisaidia Serikali.

Mwambe ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa Aprili 20, 2018 bungeni mjini Dodoma wakati Mchungaji Getrude akitoa maoni yake kuhusu bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto mwaka 2018/19.

“Mheshimiwa Spika napenda kujua kama kanisa la mama Rwakatare kuna maombi ya kuponya watu ukimwi ili kuweza kuisaidia Serikali,” amesema Mwambe.

Baada ya taarifa hiyo Mchungaji Rwakatare amesema, “Mambo hayo yapo wewe walete tu.”