Mbasha afunguka juu ya tuhuma za kumpa mimba binti Agness

Msanii wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha amesema amesikitishwa na taarifa alizozipata kuwa amempa ujauzito msichana anayevuma kwenye mitandao ya kijamii Agness na kudai hana mahusiano yeyote na mtu huyo zaidi ya kumfahamu kupitia mitandaoni

Mbasha amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana baada ya kuwepo na tetesi za muda mrefu zinazozidi kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa zinadai kuwa wawili hao wana mahusiano ya kimapenzi na mpaka kufikia hatua ya kukubalia kupeana ujauzito.
"Agness mimi namfahamu kama shabiki yangu kupitia mitandao ya kijamii. Sasa sielewi mambo yamegeuka vipi mpaka kufikia hatua ya kuambiwa mimi nina mahusiano naye. Sijawahi kuwa na mahusiano na Agness na wala sijawahi kuwa na chochote kile kinachoashiria mapenzi", amesema Mbasha.
Pamoja na hayo, Mbasa ameendelea kwa kusema "sitegemei kupata naye mtoto kama watu wanavyosema kwa kuwa sina mahusiano nae kwa vyovyote vile huyo msichana ni shabiki wangu tu".
M
Bofya hapa kuangalia video

No comments