kesi ya Nabii Tito kusogezwa mbele kidogo!

 DODOMA!
HUKUMU ya kesi ya Tito Machibya (maarufu Nabii Tito)ambayo ilikuwa itolewe maamuzi jana iliahirishwa hadi aprili 20 mwaka huu kutokana na hakimu anayehusika na kesi hiyo kuwa na dharura.

Akitoa maelezo mahakamani hapo Mwanasheria wa serikali Judithi akyusa mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Godfrey Pius alisema kesi hiyo ilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa maamuzi madogo kuhusu kesi ya mtuhumiwa huyo.

Mwakyusa alisema kesi ya Tito Machibya ambayo ilikuwa itolewe maamuzi jana mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha lakini anadharura.

“Mheshimiwa Hakimu shauri hili limeletwa kwako kwa ajIli ya kuahirishwa kutokana na Karayemaha kuwa na dharura ”alisema Mwakyusa.

Kwa upande wake hakimu mfawidhi wa mahakama Godfrey Pius aliahirisha kesi hiyo hadi aprili 20 mwaka huu itakapoletwa tena kwa ajili ya maamuzi hayo.

Pius alisema kutokana na mtuhumiwa kuwa yupo rumande atarudishwa huko hadi tarehe hiyo kwa ajili ya maauzi madogo ya kesi inayomkabili.

Wakati wa kuahirishwa kesi hiyo mtuhumiwa nabii Tito alikuwepo mahakamani hapo lakini baada ya kuahirishwa alirudishwa rumande hadi aprili 20 mwaka huu atakapofikishwa tena mahakamani.

Aprili tan mwaka huu Hakimu Karayemaha alisema mahakamaini hapo kuwa wamepokea taarifa ya kitabibu kutoka taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga inayomhusu Mchibya na maamuzi yangekuwa jana aprili 13.

Mapema februari mwaka huu Nabii Tito alidai mahakamaini hapo kuwa yeye anamatatizo ya akili yaliyosababisha kutaka kujiua na hivyo mahakama kuamuru akachukuliwe vipimo ili kupata uhakika wa juu ya afya ya akili.

Nabii Tito anashtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua kwa kujikata na wembe na kujijeruhi kwenye maeneo ya tumbo Januari 25, mwaka huu katika mtaa huo wa Ng’ong’ona alipokwenda kukamatwa na polisi.