BONDIA HASSAN MGAYA AFARIKI DUNIA
Bondia aitwaye Hassan Mbaya amefariki baada ya kucheza pambano lake la mwisho Desemba28, 2024. Bondia Mgaya alipigwa Technical Knock out (TKO) raundi ya 6 lililofanyika Tandale kwa Mtogole katika ukumbi wa Dunia Ndogo.
Bondia huyo alipoteza fahamu na kudondoka baada ya dakika chache, alipelekwa Hospitali ya Sinza kwa ajili ya matibabu, hali yake ilikuwa mbaya zaidi hivyo alikatiwa rufaa na kupelekwa hospitali ya Mwananyamara na huku ndipo umauti ulipomkuta.
Binago Blog inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na Bondi ya ngumi kwa ukujumla na wote walioguswa na msiba huu.
Post a Comment