Barbra Gonzalez kachangia makubwa kwenye soka la Tanzania. UKWELI HUU HAPA
𝗔𝗛𝗦𝗔𝗡𝗧𝗘 𝗗𝗔𝗗𝗔 𝗨𝗠𝗘𝗪𝗘𝗞𝗔 𝗛𝗜𝗦𝗧𝗢𝗥𝗜𝗔
➪Kuna msemo unasema “Kama huna maneno ya kueleweka tenda matendo yatakayoweza kukuelezea kesho” hiki ndio alichokifanya Barbra Gonzalez Mtendaji mkuu wa zamani wa Simba SC Tanzania.
➪Wakati anaingia ndani ya Club ya simba moja ya lengo lake lilikuwa kuifanya club ya Simba kuwa moja ya timu yenye thamani kubwa Afrika kama vile Al Ahly na vilabu vingine.
➪Hakulijua soka sana ila alikuwa ni mzuri kwenye Biashara na mahusiano ya soka katika ya Simba sc na vilabu na taasisi kubwa za soka Afrika ná Duniani.
➪Barbra alisimamia mikataba na thamani ya mikataba ya biashara na watumishi ndani ya Simba sc ili kujenga na kulinda thamani ya club ya Simba sc.
➪Maneno yake hayakueleweka ila matendo yake kwa sasa yanajielezea kwa kila mwana Simba sc kwa kuwa Simba sc sasa ni moja ya nembo zenye thamani kubwa Afrika.
➪Barbara aligomea mkataba wa Azam Tv kwa kusema nembo ya Simba haiwezi kuwa sawa na vilabu vingine tanzania,aligomea mkataba wa jezi wa kampuni anayomilikiwa na familia ya Dewj aligomea mkataba wa BM3 aligomea mkataba wa Tanzania Football Federation Vs GSM.
➪Hapa kwenye swala la mikataba ndipo alipojitengenezea maadui wengi ndani na nje ya Simba na ndio alipotengenezewa zengwe ni wahuni wa mjini ili aondoke.
➪Barbra alikuwa na uwezo mzuri wa kutafsiri vitu na mambo pia alijua kuipambanua Thamani ya nembo ya Simba sc.
➪Ila kuwa zaidi Barbra mahusiano yake aliyoyatengeneza kwa Club ya Simba sc ilisaidia sana Simba sc kupata nafasi ya kushiriki African Football league kwa kuwa tayari aliweka Simba sc kwenye muonekano wa kibiashara zaidi.
➪Barbra yeye hakujua soka na mbinu zake ila alijua biashara ya soka na njia zake kwa uwezo wake wa biashara kama Barbra angeendelea kuwepo Simba sc basi kwa hivi sasa Simba sc ingekuwa na nembo yenye thamani mara mbili ya sasa.
➪Wahuni wa 10% ndio waliungana kumuondoa Iron lady kwenye soka letu linalohitaji watu wenye weledi na biashara kuliko mbinu za soka lenyewe.
➪(AFL)Barbara alichangia kwa kiasi kikubwa kuwashawishi Caf kuichagua Simba sc iwepo, nyakati zake milango ya Caf ilikuwa wazi sana na Simba sc muda mwingi walikuwa na nafasi ya kuingia ndani kirahisi.
Post a Comment