AMKA NA BWANA LEO 10/06/2022

✍🏽✍🏽

KESHA LA ASUBUHI 

IJUMAA, JUNI 10 2022

KANUNI ZA INJILI LAZIMA ZITUONGOZE 

Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? Luka 13:7.

✍🏽 Bwana angefurahi kuwa na watu Wake wanaowajali zaidi kuliko walivyo sasa, wenye huruma na wanaosaidiana zaidi. Upendo wa Kristo unapokuwa moyoni, kila mmoja atazingatia masilahi ya wengine kwa upole. Ndugu hawatamdanganya yeyote katika shughuli za biashara. Hawatatoza riba kubwa kwa sababu wanawaona kaka au dada zao mahali pa karibu ambapo wanaweza kupata msaada.

✍🏽 Wale watakaotumia mahitaji ya mwingine kwa kujinufaisha wenyewe huthibitisha kabisa kwamba hawaongozwi na kanuni za injili ya Kristo. Njia yao imenakiliwa katika vitabu vya mbinguni kama udanganyifu na ukosefu wa uaminifu; na popote kanuni hizi zinapoongoza, baraka za Bwana hazitakuja ndani ya moyo. Watu kama hao wanapokea mvuto wa adui mkubwa badala ya ule wa Roho wa Mungu. Lakini wale ambao hatimaye wataurithi ufalme wa mbinguni sharti wabadilishwe na neema ya Mungu. Ni lazima wawe safi moyoni na maishani na wenye tabia zenye upatanifu....

✍🏽 Utajiri wote unaoweza kujilimbikizia, hata kama iwe ni mamilioni, hautatosha kulipa fidia kwa ajili ya roho yako. Basi usidumu kuwa na moyo mgumu na kutokuamini, na... ukishindwa malengo ya neema ya Mungu; usilazimishe kutoka kwa mkono Wake usiotaka uharibifu wa mali yako au mateso ya utu wako.

✍🏽 Kuna wangapi ambao sasa wanachukua uelekeo ambao punde unaelekeza kwenye kupatilizwa kwa hukumu. Wanaishi siku kwa siku, juma baada ya juma, mwaka kwa mwaka, kwa maslahi yao ya ubinafsi. Mvuto na utajiri wao, uliopatikana kupitia ustadi na busara waliyopewa na Mungu, hutumiwa kwao wenyewe na familia zao bila kumfikiria Mfadhili wao mwema. Hakuna chochote kinachoruhusiwa kurudi kwa Mtoaji....

🔘 Mwishowe uvumilivu wake na hawa mawakili wasio waaminifu umekwisha; na analeta mipango yao yote ya ubinafsi, ya kidunia na kuikomesha ghafla, akiwaonesha kuwa jinsi walivyokusanya kwa ajili ya utukufu wao wenyewe, anaweza kutawanya; na hawana uwezo kuupinga uweza Wake.-Testimonies for the Church 5:350, 351.

MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA 

✍🏽✍🏽

MORNING DEVOTION 

FRIDAY, JUNE 10 2022

PRINCIPLES OF GOSPEL MUST CONTROL US 

Then he said to the keeper of his vineyard, “Look, for three years I have come seeking fruit on this fig tree and find none. Cut it down; why does it use up the ground?” Luke 13:7, NKJV.

✍🏽 The Lord would be pleased to have His people more considerate than they now are, more merciful and more helpful to one another. When the love of Christ is in the heart, each will be tenderly regardful of the interests of others. Brothers and sisters will not take advantage of each other in business transactions. They will not charge exorbitant interest because they see their brothers or sisters in a close place where they must have help.

✍🏽 Those who will take advantage of the necessities of another prove conclusively that they are not governed by the principles of the gospel of Christ. Their course is recorded in the books of heaven as fraud and dishonesty; and wherever these principles rule, the blessing of the Lord will not come into the heart. Such persons are receiving the impress of the great adversary rather than that of the Spirit of God. But those who shall finally inherit the heavenly kingdom must be transformed by divine grace. They must be pure in heart and life and possess symmetrical characters....

✍🏽 All the means you may accumulate, even though it should be millions, will not be sufficient to pay a ransom for your soul. Then do not remain in impenitence and unbelief, and ... defeat the gracious purposes of God; do not force from His reluctant hand destruction of your property or affliction of your person.

✍🏽 How many there are who are now taking a course which must erelong lead to just such visitations of judgment. They live on day by day, week by week, year by year, for their own selfish interest. Their influence and means, accumulated through God-given skill and tact, are used upon themselves and their families without thought of their gracious Benefactor. Nothing is allowed to flow back to the Giver....

🔘 At last His patience with these unfaithful stewards is exhausted; and He brings all their selfish, worldly schemes to an abrupt termination, showing them that as they have gathered for their own glory, He can scatter; and they are helpless to resist His power.—Testimonies for the Church 5:350, 351.

MAY GOD BLESS YOU ABUNDANTLY

No comments