ZUHURA YUNUS ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bi. Zuhura Yunus Abdallah kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu.
Kabla ya uteuzi huo, Bi. Zuhura alikuwa Mtayarishaji wa Vipindi na Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).
Bi Zuhura anachukua nafasi ya Bw. Jaffar Haniu ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Uteuzi huu umeanza Leo Tarehe 01 February 2022.
Post a Comment