DKT. TULIA ACKSON ATEULIWA KUWA SPIKA MPYA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Bunge la Tanzania limemchagua Dkt. Tulia Ackson kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dk Tulia amefanikiwa kuwagaragaza wagombea wenzake nane wanaotoka vyama vyengine vya kisiasa huku akipata jumla ya kura 376 kati ya kura zote zilizopigwa.

Tulia aliwahi pia kuwa Naibu Spika chini ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo Mhe. Job Ndugai ambae amejiuzulu mapema mwezi Januari baada ya kutokea kwa mkwaruzano kati yake na Rais Samia Suluhu Hassan.

No comments