SIMBA SC YAMSIMAMISHA MCHEZAJI WAO BERNARD MORRISON 'Bm3' KWA MUDA KWA KUTOKUWA NA NIDHAMU KLABUNI HAPO

Klabu ya Soka ya Simba SC imemsimamisha kwa muda mchezaji Bernard Morrison hadi suala lake la kinidhamu litakapopatiwa ufumbuzi.

Simba SC Imesema Morrison amekua na tabia ya kutoka kambini bila ruhusa kinyume na utaratibu.
Mara ya mwisho Morrison alitoka kambini na uongozi wa benchi la ufundi ulimpa maelekezo kuwa asirejee kambini hapo mpaka atakapoonana na Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez.

Hata hivyo Simba SC Imesema Morrison hakutiïi maagizo hayo hivyo kuendelea kukaa nje ya kambi.

Kufuatia kadhia hiyo Uongozi wa klabu umemsimamisha kwa muda na kumtaka atoe maelezo ya maandishi kwa Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, na endapo atashindwa kufanya hivyo Bodi imesema hatua zaidi za kinidhamu zitachukuliwa.

No comments