DULLAH MBABE APOTEZA PAMBANO, TWAHA KIDUKU AMPA POLE
Bondia Abdallah Pazi maarufu 'Dullah Mbabe' kutoka Tanzania amepoteza pambano lake dhidi ya Bondia kutoka nchini Congo DR, Tshimanga Katompa baada ya kupewa ushindi na majaji wote 3 (90-97, 93-94, 93-94).
Bondia kutoka Mkoani Morogoro Twaha Khassim maarufu 'Twaha Kiduku' amempa pole Bondia kutoka Jijini Dar es salaam Abdallah Pazi maarufu 'Dullah Mbabe' baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Bondia kutoka nchini Congo DR, Tshimanga Katompa jana usiku.
"Pole sana Brother huwezi kua champion bila kupoteza ata wakina Tyson walipoteza na wakajifunza ndiomana wakafanya makubwa usikate tamaa bado nafasi unayo na uwezo pia unao"
"Mchezo unamatokeo matatu (3) kushinda, kudraw na kupoteza usivunyike moyo kuanza upya sio ujinga mfano wewe ulinipiga round ya kwanza nikaanguka lakini sikukata tamaa pambana Brother ndio mchezo ulivyo."---- TWAHA KIDUKU
Post a Comment