AMKA NA BWANA LEO 10/10/2021
*KESHA LA ASUBUHI*
*_LEO NA MUNGU - Jumapili, Oktoba 10, 2021_*
*DHIFA YA NENO LA MUNGU*
*_Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa Ulimwengu. Yohana 6:51._*
✍🏼 Usalama pekee kwa kila mmoja wetu upo katika kukita miguu yetu katika Neno la Mungu na kuyasoma Maandiko, *kulifanya Neno la Mungu kuwa tafakuri yetu ya kila siku.*
🎤Waambieni watu wasilichukue neno lolote la mtu na kulilinganisha na Maneno ya ushuhuda, lakini wayasome na kujifunza wao wenyewe na ndipo watakapojua kwamba yana uwiano na ukweli. *Neno la Mungu ndiyo Kweli. Mtu mwema mtunga zaburi anatangaza, _"Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, na sheria yake huitafakari mchana na usiku"_ (Zaburi 1:2).*
👉🏽 Yeye ambaye huweka akili na moyo wake katika kazi hii hupata uzoefu thabiti na imara. *Roho Mtakatifu yuko katika Neno la Mungu.* Hapa kuna kitu hai kisichokufa kinachowasilishwa katika Yohana sura ya sita....
✍🏼 Hebu na tuliamini Neno. Yeye aulaye mkate wa mbinguni hurutubishwa kila siku, na atajua maneno haya yana maana gani, *_"Wala hamna haja ya mtu kuwafundisha."_*
👉🏽Tunayo mafundisho safi kutoka katika kinywa chake Yeye anayetumiliki, ambaye alitununua kwa gharama ya damu yake. *Neno la Mungu la thamani ni msingi imara kujenga juu yake.*
*👉🏽Wakati wanadamu wanakujia na dhana zao, waambie kwamba Mwalimu Mkuu amekuachia Neno lake, ambalo thamani yake haiwezi kulinganishwa, na kwamba amemtuma msaidizi kwa jina lake pekee, ambaye ni Roho Mtakatifu. _"Atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia"_ (Yohana 14:26)....*
*✍🏼 Hapa mbele yetu imewasilishwa karamu iliyo kuu, ambayo wale wote wanaomwamini Kristo kuwa Mwokozi wao binafsi wataiingia. Yeye ni mti wa uzima kwa wale wote wanaoendelea kujilisha kwake....*
*✍🏼 Wale wote wanaojifunza matamko haya ya thamani watapata faraja kubwa mno. Kama watajilisha katika karamu ya Neno la Mungu, watapata uzoefu wa thamani ya juu sana. Wataona kwamba ukilinganisha na Neno la Mungu, maneno ya wanadamu ni kama makapi katika ngano.*
🔘 *Nimeagizwa na Neno la Mungu kwamba ahadi zake ni kwa ajili yangu na kwa kila mtoto wa Mungu.*
*🔘Karamu imeshaandaliwa mbele yetu, tunaalikwa kujilisha Neno la Mungu, ambalo litaimarisha misuli na mishipa ya kiroho.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*
Post a Comment