Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 23

*✍🏽✍🏽 KESHA LA ASUBUHI*

_Jumatatu; August 23, 2021_

*SOMO: KIPIMO CHA UAMINIFU*

_👉Lakini iweni wayendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Yakobo 1:22._

*😇Kwa kila nafsi Bwana anadai utumishi. Wale ambao maneno ya uzima yamefunguliwa kwao, ambao wanauona ukweli, na kujitoa mwili, nafsi, na roho kwa Mungu wataelewa maneno ya Mwokozi, "Leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu" (Mathayo 21:28),  kuwa ni sharti muhimu, lakini siyo lazima. Mapenzi ya Mungu yanatambuliswa katika Neno lake, na wale wanaomwamini Kristo wataitenda imani yao. Watakuwa watendaji wa Neno.*

_⚖️Kipimo cha uaminifu sio kwa maneno, bali ni kwa matendo. Kristo hasemi kwa mtu yeyote, "Je mnasema nini zaidi ya wengine?" bali, "Mnafanya nini zaidi ya wengine?"? Maneno yake yamejaa maana ya kina, "Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda" (Yohana 13:17). Maneno hayana thamani yoyote isipokuwa yamesemwa Kwa uaminifu na ukweli. Kipaji cha maneno kinafanywa kuwa chenye ufanisi na cha thamani pale yanapoambatana na matendo sahihi. Ni muhimu sana kwa kila nafsi kusikia Neno na kuwa mtendaji wake._

😇"Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba: maana mlango ni mpana, na njia ni pana, iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo" (Mathayo 7:13) ....

*🌳Tunao ushahidi kwamba wadanganyifu wengi ulimwenguni, watu ambao wanasema, "Nitakwenda, Bwana," lakini hawaendi. Wanaweza kusema maneno laini, na kutoa hotuba zilizo nzuri; lakini wanadanganya; wanadhihirisha katika maisha yao kwamba maneno yao hayajatoka kwa Mungu. Maisha ya vitendo ni ishara halisi ya tabia. Kwa maneno na kazi zetu tunadhihirisha  kwa ulimwengu, kwa malaika, na kwa watu kuwa tumwamini Kristo kama Mwokozi binafsi.*

_👉Matendo mema hayanunui upendo wa Mungu, lakini yanadhihirisha kuwa tunao upendo huo. Ikiwa tutasalimisha mapenzi na njia yetu kwa Mungu, hatutafanya kazi ili kupata upendo wa Mungu; tutazitii amri za Mungu kwa sababu ni sahihi kufanya hivyo. Yohana mwanafunzi  wa Yesu aliandika

Post a Comment

0 Comments