Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapongeza Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ubunifu na kurejesha ari na hamasa ya michezo kwa Taifa ikiwa ni pamoja na kuyatangaza na kuchechemsha mashindano kwa Shule za Msingi na Sekondari ambayo yalifanyika mwaka huu katika Mkoa wa Mtwara.
Akiongea katika hafla maalum ya kukabidhi Kombe la ushindi la Michuano ya Mpira wa Miguu kwa Vijana wrnye Umri Chini ya Miaka 23 kwa Mataifa ya Ukanda wa Aftika Mashariki (CECAFA) iliyofanyika jana Agosti 22, 2021 Ikulu Dar es salaam, Rais Samia alisema kuwa umuhimu wa michezo kwa sasa sio tu katika kuimarisha afya lakini pia inatoa ajira na kulitambulisha Taifa kwenye Mataifa mengine duniani.
“Nitumie fursa hii kuwapongeza Viongozi wa Wizara yenye dhamana kwa kushirikiana na Wizara nyinyine kurejesha upya hamasa ya michezo ya shule za Msingi na Sekondari na pia kwa mipango yenu ya kufufua mashindano ya Taifa yatakoshindaniwa na Mikoa kwenye michezo mbalimbali. Aidha nawapongeza kwa kubuni wazo la kuanzisha Tamasha la kila mwaka ‘Tanzania Sports Festival’, hatua hii naamini itasaidia kukuza sekta ya michezo nchini”, alisema Rais Samia.
Akiongelea mipango ya Serkali katika kuunga mkono sekta ya michezo, Rais Samia alisema Serikali imedhamia kwa dhati kukuza sekta hiyo nchini ambapo tayari imeanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Michezo kwa ajili ya kusaidia timu za Taifa na kwa mwaka 2021 mfuko huu umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 1.5 na kuahidi kuendelea kuutunisha mfuko huo kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.
Alisema mipango mingine ni pamoja na kuondoa tozo na ushuru mbalimbali kwa vifaa vya michezo ikiwemo nyasi bandia, ujenzi wa viwanja vitatu vya kisasa vya mazoezi ambavyo vitajengwa katika Mikoa ya Dar es saalam, Dodoma na Geita lakini pia ujenzi wa kituo cha kulea vipaji vya michezo (Sports Academy) mkoani Mwanza.

0 Comments