ALI SULEIMAN SALULA ASAINI AZAM FC
Azam FC imeingia mkataba wa miaka miwili na golikipa, Ahmed Ali Suleiman 'Salula', akitokea KMKM ya Zanzibar.
Golikipa huyo mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.
Salula ni mmoja wa makipa hodari, akiwa ndio tegemeo katika timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes', anakuja kuongeza nguvu katika eneo la langoni kwenye timu ya Azam FC.
Huo unakuwa usajili wa saba kwa Azam FC kuelekea msimu ujao, wakiwa na nia ya dhati ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CC).
Wachezaji wengine waliosajiliwa ni beki wa kushoto, Edward Manyama, kiungo mkabaji, Paul Katema (Zambia), viungo washambuliaji, Charles Zulu (Zambia), Kenneth Muguna (Kenya) na washambuliaji Rodgers Kola (Zambia), Idris Mbombo (DRC).

Post a Comment