WALIOPONA CORONAVIRUS WAANZA KUPOTEZA KUMBUKUMBU

Karibu theluthi moja ya wagonjwa wa coronavirus waliopona huko Hong Kong nchini China, wameripoti kupoteza kumbukumbu. ⁠
Asilimia kama hiyo ilipata hisia za unyogovu na wasiwasi ambao uliendelea kwa miezi kadhaa baada ya kupona.
Baadhi ya wagonjwa 128 waliopona waliohojiwa na timu kutoka Chuo Kikuu cha China walisema wamejikuta wakisahau majina ya marafiki au wakishindwa kuzingatia majukumu, wakati mgonjwa mmoja mzee hakukumbuka kabisa njia ya kurudi nyumbani kwake

"Haya ni matokeo ya awali tu, na utafiti bado haujakamilika… lakini tunaweza kusema kuwa matokeo haya hayakuwahi kutokea na hayajatarajiwa," alisema Dk Arthur Mak Dun-ping, ambaye anaongoza utafiti.

No comments