SIKUKUU YA EID-EL-ADH'HAA KUFANYIKA TAREHE 21/07/2021
Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally Mbwana ametangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Adh'haa itakuwa tarehe 21/07/2021 siku ya Jumatano ambayo ndiyo itakuwa siku ya mapumziko kitaifa.
Maadhimisho ya Sikukuu ya Eid El-Adh'haa kitaifa yatafanyika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo Swala ya Eid Kitaifa itaswaliwa katika Msikiti wa Mtoro kuanzia saa 1:30 asubuhi na Baraza la Eid litafanyika hapo hapo mara tu baada ya Swala hiyo.
Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania Mh. Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana amewatakia Waislamu na wananchi wote Sikukuu njema na amewaomba kusherehekea kwa Salama na Amani huku tukiendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa CORONA (Uviko-19).
Post a Comment