WALIOKOSA FURSA KWENDA HIJJA WAPEWE MOYO-HUSSEIN MWINYI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amezitaka taasisi zinazowasafirisha Mahujaji pamoja na Masheikh na Walimu kuendelea kuwapa moyo Waislamu waliokosa fursa ya kwenda Hijja kutokata tamaa.
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Wete Pemba katika hotuba yake ya Baraza la Idd el Hajj aliyoitoa kwa wananchi.
Katika maelezo yake, Alhaj Dk. Miwnyi alieleza kwamba kwa wale ambao walifikia hatua ya kutoa gharama za safari waondolewe shaka kuwa fedha zao ziko salama hadi Mwenyezi Mungu atakapowezesha kwenda kutimiza wajibu huo kama walivyoazimia.
Hivyo, aliwataka waumini kufuata mafundisho ya Uislamu katika hali kama hiyo waendelee kuwa na subira, wasichoke kuomba dua na kubaki katika Imani na uchamungu.
Aidha, Alhaj Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali ya Saudia Arabia lilitangaza kuwazuwia Waislamu kutoka nchi za kigeni kwenda kuitekeleza ibada ya Hijja kwa mwaka huu kutokana na kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa COVID 19 katika Mataifa mbali mbali duniani.
Alisema kuwa hali hiyo kwa mara nyengine imesababisha Waislamu wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla kwa mwaka wa pili mfululizo wamekosa fursa ya kwenda Hijja licha ya maandalizi ambayo walikuwa wameshayaanza.

Post a Comment