NDEGE YA SKYWARD EXPRESS YAANGUKA CHINI

Ndege ya Skyward Express nchini Kenya, imeanguka katika kituo cha kijeshi nchini Somalia.

Ndege hiyo ilikuwa na abiria 37 na wahudumu 3 ndani ambao wote walinusurika na majeraha kidogo.

Ndege hiyo De Havilland #Canada #DHC-8-100 yenye nambari ya usajili, 5Y-GRS ilitua kwa kuangukabkatika uwanja wa ndege wa jeshi la Burache huko Elwak karibu na Somalia ikitokea Wilson, Nairobi kuelekea Uwanja wa Ndege wa nMandera, Kenya wakati tukio hilo lilipotokea.

No comments