TUTASHUGHULIKIA STAHIKI ZA VIJANA VIWANDANI-JOKATE
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam amesema, wamekuwa wakipokea malalamiko mengi sana hasa ya vijana Kuhusu kunyimwa au kucheleweshewa stahiki zao na waajiri ndani ya wilaya ya Temeke.
Jokate amesema, waliamua kutembelea kiwanda cha KTM kilichopo eneo la Mission Kata ya Mbagala ambapo walibaini changamoto wanazopitia wafanyakazi wa kiwanda hicho ikiwemo kucheleweshwa kwa mishahara, mazingira mabaya ya kazi, na maswala mbalimbali ya kodi pamoja na mapato.
"----->Pamoja na kushughulikia stahiki za vijana wafanyakazi ambazo wamiliki wa kiwanda tayari wameahidi kuanza kuzishughulikia"---- JOKATE

Aidha, ameelekeza idara na vitengo vya Biashara, Mazingira na Uhamiaji na Afisa Kazi wa Manispaa pamoja na TRA mkoa wa Temeke kuchukua taarifa na hatua stahiki baada ya kukuta kiwanda kinafanya shughuli zingine kinyume na taratibu zilizopo.
Post a Comment