TPBL YASOGEZA MBELE KWA SIKU MOJA MZUNGUKO WA 33 VPL

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesogeza kwa siku moja mbele michezo yote ya mzunguko wa 33 wa Ligi Kuu ya Vodacom 2020/2021 ambapo sasa itachezwa Julai 15, 2021 badala ya Julai 14 kama ilivyopangwa hapo awali.

Mabadiliko haya yametokana na ombi la timu ya Polisi Tanzania kusogezewa angalau kwa siku moja mbele mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar FC baada ya timu hiyo yenye makao yake makuu mjini Moshi, kupata ajali ya barabarani Julai 9 iliyosababisha majeraha kwa baadhi ya wachezaji wao.

Ili kupata uwiano sawa wa michezo kuelekea kumalizika kwa msimu, Bodi ya Ligi imeamua kusogeza michezo yote ya mzunguko wa 33 kwa siku moja mbele hivyo timu zote zitacheza mechi za mzunguko huo Julai 15 kama ilivyoelezwa hapo juu.

Tunawatakia nafuu ya mapema wachezaji na maofisa wote wa Polisi Tanzania FC waliopata majeraha katika ajali hiyo na kila la kheri kwa
timu zote katika maandalizi ya kuelekea michezo iliyosalia.

No comments