MAJALIWA ATOA SIKU 7 UCHUNGUZI SOKO LA KARIAKOO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku saba kwa kwa timu iliyoundwa kuchunguza chanzo cha ajali ya moto katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Ametoa agizo hilo mapema leo asubuhi wakati akizungumza na wahanga wa moto huo, na kusema timu hiyo itatoa pia ushauri wa kitaalamu.

Ameongeza kuwa ikiwa itabainika kuna hujuma zozote zimefanyika serikali haitasita kuchukua hatua stahiki.

Moto huo ambao umeteketeza maduka ya wafanyabiashara katika soko hilo ulinza kuwaka majira ya saa mbili usiku Julai 10, 2021.

No comments