SERIKALI KUANZISHA SHULE MAALUM ZA MICHEZO
Serikali imesema ipo kwenye hatua za mwisho za kuanzisha shule maalum za michezo, za msingi na sekondari, katika mikoa yote nchini lengo likiwa ni kuwa na shule na vituo maalum vya kuendelezea vipaji vya michezo (sports academies).
Akizungumza kwenye Sherehe za kufunga mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) mjini Mtwara leo Julai 2,2021 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Shule hizi zitakuwa zinalea na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali, na Serikali itakuwa inasimamia kwa ukaribu, kuhakiksiha kuwa vituo vya michezo vya shule za msingi na sekondari, vinapatiwa mahitaji muhimu yatakayo saidia katika kuendeleza vipaji hivyo.
Amesema Serikali kupitia Chuo cha Maendeleo ya Michezo – Malya, inaanzisha kituo maalum cha michezo cha kuendeleza vipaji (Centre of Sports Excellency), vitakavyokuwa vinapatikana kutokana na mashindano haya, na maeneo mengine mbalimbali nchini.
« Chuo cha maendeleo ya michezo Malya kimeanzisha mafunzo ya astashahada, ili kupanua wigo wa wanufaika wake, pia kimefungua kituo cha mafunzo Dar es salaam na Ruvuma, ili kusogeza huduma kwa wananchi wengi zaidi. Ni matumaini yetu kuwa, kupitia Chuo hiki, tutaweza kupunguza pengo la watalaam, na walimu wa Michezo ambalo tunalo hivi sasa amesisitiza Mhe. Bashungwa
Katika mashindano ya mwaka huu ya UMISSETA mkoa wa Dar es Salaam umeibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika michezo yote.
Pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu, kwa maelekezo yake ya kuondoa kodi ya VAT, katika kununua na kuingiza nyasi bandia nchini, ili tuweze kujenga na kukarabati miundombinu yetu ya michezo.
Wizara yangu imejipanga kuanza kuhamasisha taasisi na wadau mbalimbali, kuchangamikia fursa iliotolewa kwa kuboresha miundombinu ya viwanja vyao. Nimatumaini yetu kuwa, kwa hatua hii tunakwenda kuimarisha, na kuboresha mioundombinu ya michezo nchini amefafanua Mhe. Bashungwa.

Post a Comment