RAIS HUSSEIN MWINYI AKAGUA UJENZI KATIKA SOKO LA MALINDI

Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Malindi pamoja na kuzungumza na wavuvi ili kujua changamoto zinazowakabili. 

"Nimetumia fursa hiyo pia kuwaeleza kuwa Serikali imekusudia kuhakikisha wavuvi wanatumia vyombo vikubwa na vya kisasa vyenye uwezo wa kuwafikisha mbali ili waweze kupata tija kutokana na kazi wanazofanya"--- MWINYI

Aidha, Rais Hussein Ali Mwinyi amesema serikali haina azma ya kuwapa watu wengine nyumba za wakaazi wa Mji Mkongwe, bali inalenga kuzinusuru nyumba hizo na kuanguka kutokana na kukabiliwa na hali mbaya ya ubovu.

"Serikali inakusudia kuurekebisha Mji Mkongwe na kuwa Mji wenye ‘Master Plan’ na utakaokuwa na miundombinu yote muhimu itakayokidhi mahitaji."--- MWINYI

No comments