NENO KUU MAKAMBINI LEO 3

SOMO : SISI URAIA WETU UKO MBINGUNI
Trh 3 July 2021, Jumamosi
Makambi- Tanga Jiji
Pr. Godwin Lekundayo.

😋watu hupokea mahubiri na injili kwa nia zao wenyewe, kwa ajili ya miujiza, kupanda vyeo, maisha yao yanyooke...n.k. Na hii ndio maana madhehebu ya kikristo yapo mengi zaid.

✓ kuna injili mbili 
1. Maisha haya... Hii ni faida ya papo hapo.
2. Milele...hii itakupa faida badae.

✓Wapo watu waliobarikiwa katika maisha ya sasa ni akina Daudi, suleimani, yohana mbatizaji, petro n.k na pia wakabarikiwa kwa ajili ya badae. Usipokee injili kwa ajili ya manufaa ya sasa. Mungu akikupa kibali cha kubarikiwa sana kwa maisha haya inabidi umpe Mungu utukufu.

✓Matendo ya Mitume 1:6-7
Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?

Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.

✓Matendo ya Mitume 1:8-11
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.

Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,

wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

✓baada ya Yesu kusulubiwa , kufufuka na kuwatokea watu kila mahali alijidhihilisha kwao kwa njia ya kumega mkate kwao.... Kumbe Yesu anajidhihilisha kwetu kwa kusoma Neno lake.

✓Tutapokea Nguvu akiisha kuja kwetu Roho Mtakatifu, na huu ni mkazo wake Yesu juu yetu. Na huyu Roho Mtakatifu atafanaya mambo mawili...
1. Kutufanya sisi kufaa kuwa rahia wake
2. Kuwaandaa wengine wafae kwa ajili ya ufalme wa Mungu.

✓ Mara nyingi tunashindwa kuipokea nguvu hiyo kwa sababu tumeshindwa kuangamiana sisi kwa sisi, hata wanafunzi wake waliungamiana wao kwa wao kila mtu na mwenzake.

✓E.G.W anasema kuna roho mahali fulani wanahitaji kumpokea Roho Mtakatifu. Hivyo tunaishi kwa ajili ya wengin. 

✓Tazama;  hauishi ili uolewe, usome, ujenge. Wewe unaishi kwa sababu ya vitu viwili.
1. Kufanya sehemu yako kwa wengine..sadaka yako na mali yako
2. Unaishi maana kuna jambo fulani hujaliweka sawa mahali fulani. Yesu anataka kuukata mti lkn sauti ya Roho Mtakatifu inasikika  kuwa acha usiukate, usiondoe maana huenda utachipua tena na kuzaa matunda. Hii ndiyo kazi ya Roho Mtakatifu kwetu akitubembeleza n kutusihii.

✓Unapokataa kuisikila sauti ya Mungu...itafikia mahali atanyamaza na hapatakuwa na atakae kushawishi kuungama dhambi zako. Na kama atanyamaza hutatubu.

✓Wafilipi 3:20-21
Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;

atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.

✓Paulo anasema...Usituone hivi; mara tunaumwa, tunaenda makazini, kusoma n.k ..lkn sisi wenyeji wetu uko mbinguni.

✓Tunaishi Tanzania: lkn wapo ambao wanaishi hapa na urahia wao uko mbinguni. Duniani hapa kuna nchi haziruhusu kuwa na urahia ktk nchi mbili...lkn kwa Mungu wetu inaruhusiwa.

✓kuwa na utamaduni wa kuongea na Mungu kila wakati ukiunganishwa nae kwa njia ya maombi. Kumbuka ulipo urahia wako ndipo unapopaswa kuishi.

✓Kwa waafrika mtu aliyelipiwa mahari haruhusiwi kuolewa kwingine..! Hata sisi tumeshalipiwa mahari kwa njia ya Damu pale msalabani. Na ananisubiri tu kuja kunichukua ili nikaishi makao ya kudumu!.

✓Unajua safari ya kwenda mbinguni ina uchaguzi...haulazimishwi kwenda.

✓Ufunuo wa Yohana 21:16-18
Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.

Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.

Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.

✓Yesu atashuka kuwachukua watu wake na kwenda nao mbinguni lkn baada ya miaka 1000 litashuka hapa Duniani ambapo pameshasafishwa. 

✓Yaspi ni madini ambayo yanakufanya uone zaidi ya kioo na hapo utaweza kuwaona watu walio nje ya jiji baada ya ufufuo kwa maana waliukataa huo mwaliko wa kuuchagua mji huo.

✓ Utajiuliza maswali mengi sana kuona uliyemfaham akiwa nje ya jiji kutokana na uchaguzi wake. Fanya uchaguzi mzuri wa kuingia katika jiji hili.
🧠Barikiwa sana. Limenukuliwa vizuri na Mugeta Tz.🧠

No comments