MWONGOZO WA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA COVID-19

Mwongozo huu unalenga kuweka mazingira wezeshi katika maeneo ya Taasisi za elimu ikiwa ni pamoja na; Vyuo, shule za sekondari, shule za Msingi, shule za awali na vituo vya kulelea watoto wadogo mchana (Day care centres) kabla ya wanafunzi kurejea shule na vyuo na kuendelea na masomo katika kipindi hiki cha mlipuko wa Homa kali ya Mapafu inayosababishwa na Virusi aina ya Corona.

Katika kufanikisha uwepo wa mazingira hayo, Mwongozo umezingatia maeneo makuu manne ambayo ni Maandalizi ya mazingira na taasisi za elimu kabla ya kufunguliwa, Uchunguzi wa Afya, Usafiri wa kwenda na kurudi shule na vyuo na Mazingira ya kujifunzia.

Maandalizi ya Mazingira ya Taasisi za elimu kabla ya kufunguliwa, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara zote zinazosimamia vyuo na taasisi za mafunzo wanashauriwa kuhakikisha mazingira salama ya shule, vyuo na Taasisi za elimu kabla wanafunzi kurejea ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19. Katika kuandaa mazingira@Prof.Abel Makubi,Katibu Mkuu-Afya.

No comments