Advertisement

Responsive Advertisement

MUONGOZO WA KUSOMA BIBLIA LEO 19

😍*MWONGOZO WA KUJIFUNZA BIBLIA* 

*SOMO;WITO WA KUAMKA* 

*Katikati ya moja ya nyakati mbaya zaidi katika maisha ya Daudi kuna habari njema: Mungu anamtuma nabii Wake. Nathani na Daudi walifahamiana vizuri. Hapo kabla, Nathani alimshauri Daudi kuhusu mpango wake wa kujenga hekalu (2 Sam. 7). Sasa, hata hivyo, nabii anakuja na kazi tofauti ya kufanya kwa mfalme wake.* 

*Kwa nini unafikiri Nathani anachagua kusimulia kisa badala ya kumtaja na kumwaibisha Daudi mara moja? Soma 2 Samweli 12:1—14.* 

🔹Nathani alijua cha kusema, naye alikisema kwa namna ambayo Daudi angeelewa. Alisimulia kisa ambacho Daudi, aliyekuwa mchungaji, angekielewa nacho. Alijua utambuzi mpana sana wa Daudi kuhusu haki na uadilifu. Hivyo, kwa uelewa huu, mtu angeweza kusema kwamba Nathani alitega mtego ambao Daudi aliuingia moja kwa moja.

🔹Daudi alipotoa hukumu ya kifo chake mwenyewe pasipo kujua, Nathani anamwambia “ ‘Wewe ndiwe mtu huyo’ ” (2 Sam. 12:7). Kuna njia nyingi za kusema “Wewe ndiwe mtu huyo.” Mmoja anaweza kusema kwa sauti, mwingine anaweza kushutumu na kusonda kidole katika uso wa yule mtu mwingine, au mwingine anaweza kuonesha kusikitishwa na kujali. Maneno ya Nathani yalitiwa neema. Kwa wakati huo, Daudi atakuwa alihisi uchungu ambao Mungu anauhisi wakati mmoja wa wana au binti zake kwa kujua wanatoka nje ya mapenzi yake. Kitu kiligusa akili ya Daudi. Kitu kiliraruka katika moyo wake.

*Kwa nini Daudi anajibu kwa kusema: “Nimemfanyia BWANA dhambi” badala ya, “Nimemfanyia Bath-sheba dhambi” au “Mimi ni mwuaji” (2 Sam. 12:13; tazama pia Zab. 51:4)?* 

🔹Daudi alitambua kwamba dhambi, inayofanya mioyo yetu ikose utulivu, kwanza kabisa ni kumchukiza Mungu, Muumbaji na Mwokozi. Tunajiumiza wenyewe; tunawaathiri wengine. Tunaleta aibu kwa familia zetu au makanisa. Lakini hatimaye, tunamuumiza Mungu na kugongomelea msumari mwingine katika mti unaoparuza kuelekea mbinguni juu ya Golgotha.

🔹“Kemeo la nabii liliugusa moyo wa Daudi; dhamiri iliamshwa; hatia yake ilionekana katika ukubwa wake wote. Nafsi yake iliinamishwa katika toba mbele za Mungu. Kwa midomo inayotetemeka alisema, ‘_ BWANA dhambi._’ Mabaya yote waliyotendewa wengine hutoka kwa walioumizwa na kumfikia Mungu. Daudi alitenda dhambi mbaya sana, juu ya Uria na Bath-sheba pia, na alilihisi sana hili. Lakini kwa ukubwa sana ilikuwa dhambi yake dhidi ya Mungu.” _—Ellen G. White, Patriarchs and Prophets, uk. 722.`

*NAKUTAKIA TAFAKARI NJEMA*

Post a Comment

0 Comments