Familia katika kijiji cha Obumba, Kaunti ya Kisumu nchini Kenya, inaomboleza kupoteza jamaa yao baada ya kujiua kwa kujinyonga.
Joshua Odhiambo Ouma mwenye umri wa miaka 23 alijiua kwa kujinyonga kwenye nyumba ya jirani baada ya ndugu zake kukataa mipango yake ya kuuza kipande cha ardhi ya familia.
Kulingana na mama wa marehemu, mtoto wake alitaka kuuza kipande hicho cha ardhi ili kupata pesa za kupata leseni ya kuendesha gari.
Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Kisumu Samuel Anampiu alisema familia hiyo ilikuwa na mkutano Jumapili juu ya suala hilo lakini ndugu zake walikataa ombi lake.
0 Comments