MAKAO MAKUU YA TAWA KUHAMISHIWA DAR ES SALAAM

Waziri ya Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbari amesema Wizara ya Maliasili na Utalii iko katika mchakato wa kuhamisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Jijini Dar es Salaam, ili kuiwezesha kuwahudumia wateja wake ambao kwa zaidi asilimia 90 wanatoka katika Jiji hilo

Ameyasema hayo  wakati alipotembelea Chuo cha Viwanda vya Misitu ( FITI) kuzungumza na uongozi wa Chuo hicho

Amesema ofisi ya Morogoro haitafungwa bali kutakuwa na ofisi ndogo ya TAWA

Amesema makao hayo ni lazima yawe Dar es Salaam na hivyo TAWA hakuna haja ya kuhamia Dodoma kwa vile wateja wake wapo Jijini Dar es Salaam

" TAWA ni taasisi inayofanya biashara hivyo ni lazima iwafuate wateja wake walipo, alisisitiza Dkt.Ndumbaro

No comments