Ameyasema hayo wakati alipotembelea chuo hicho na kuzungumza na uongozi, na kuongeza kuwa kutokana na uwepo wa misitu huko Mafinga hakutakuwa na haja ya kutumia gharama za kusafirisha magogo kwa ajili ya matumizi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na misitu chuoni hapo.
“Mafinga ndio sehemu yenye viwanda vingi vya mbao vya watu binafsi, na hiyo itasaidia Wanafunzi kufanya mafunzo kwa vitendo katika viwanda hivyo na tunazo hekta 120 za Serikali ambazo sio za kununua na kwamba suala la kuhama haliepukiki.” amesema Waziri Ndumbaro
Amebainisha kuwa chuo cha FITI Moshi hakitafungwa bali kitakuwa ni tawi na kwamba hakitahamishwa
0 Comments