KIGWANGALLA ASIKITISHWA NA KIFO CHA ELISHILIA KAAYA

"Nimesikitishwa sana na taarifa za kifo cha ndugu yangu Elishilia Kaaya"

"Alikuwa mtu mwema na mzalendo wa kweli. Alikuwa mwana CCM Kwa imani kabisa, na aliipenda sana nchi yetu"
 
"Nilihudumu kwenye Bodi ya AICC pamoja naye akiwa Katibu wa Bodi yetu (Mkurugenzi Mtendaji wa AICC), na alitusaidia sana kutekeleza majukumu nyeti ya CCM ukanda ule kipindi akiwa MNEC"

"Leo ameondoka, namkumbuka kama miongoni mwa watu wachache walochukia ufisadi kwa dhati, akiwa miongoni mwa waadilifu, waaminifu na wachapakazi niliowahi kufanya nao kazi"

"Natoa pole kwa mkewe, wanae, Wizara ya Mambo ya Nje, AICC na wote walioguswa na msiba huu. Pumzika kwa Amani Komredi. Mungu akupe kauli thabit huko."--- @hamisi_kigwangalla 

No comments