HUSEEIN KWINYI AFANYA UTEUZI KWA MAKATIBU WAKUU, MANAIBU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kama ifuatavyo:-

1) Ndugu Mussa Haji Ali ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu.
2) Ndugu Habiba Hassan Omar ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.
3) Ndugu Issa Mahfoudh Haji ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.
4) Ndugu Aboud Hassan Mwinyi, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Anayeshughulikia (Fedha na Mipango).
5) Ndugu Mikidadi Mbarouk Mzee ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 10 Julai, 2021.
Aidha, Wateuliwa wote waliotajwa wataapishwa siku ya Jumatatu tarehe 12 Julai, 2021 Saa 4.00 Asubuhi - Ikulu Zanzibar.

No comments