FREEMAN MBOWE ASHIKILIA MKAZO WA KATIBA MPYA LEO
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amesema Katiba mpya iundwe na Bunge maalum la Katiba, na sio Bunge lililopo, amesema hawatakubali Bunge lililopo kuunda Katiba Mpya bali liundwe Bunge Maalum la Katiba.
Aidha, amesema hawatampa muda Rais Samia Suluhu Hassan, ambao aliomba kuwa afanye mambo mengine kisha Katiba itafuata.
"Tunapendekeza kuwe na bunge la Katiba na lisiwe bunge hili la sasa wala wasituambie bunge hili la sasa ndio liunde Katiba, ichukuliwe rasimu ya Warioba na Katiba na kisha iundwe rasimu ya Katiba mpya, sio gharama na tukiamua tutapata katiba mpya mwaka huu” ----> @freemanmbowetz
Post a Comment