ATMFALME AWATAKA WAZANZIBAR WAHAMIE KWA HARMONIZE

Mfalme wa miondoko ya mduara, ATMFALME kutoka visiwani Zanzibar ametumia ukurasa wake wa instagram kutoa shukrani zake kwa mashabiki, vyombo vya habari, kadhalika na HARMOMIZE kwa kumrejesha vyema kwenye ramani ya muziki kwasasa.

Pia ATMFALME awataka wazanzibar wasirubuniwe, wamuunge mkono boss huyo wa KONDEGANG kwa kiasi kikubwa kwani ana roho ya kipekee sana. Ameeleza.

"Nimekuwa nikifanya kazi kwa Kuzingatia Ukubwa wako na Heshima ya Watu wetu wote Nichukue nafasi hii kukushukuru wewe HARMONIZEBna kila shabiki wako na Uwongozi Mzima Kwa kufanya Leo AT azungumzike atizamike Upya pamoja na kuwashukuru kwa Dhati Media's Zote kwa kila sekta na Fans wangu na Wasanii wenzangu wote wanaonipenda na wasionipenda mimi niseme Shukran sana sana Mubarikiwe.

Naomba nitoe Ahadi ya kufanya Kazi Nzuri zaidi na kwa uadilifu. Wazanzibar Naomba Niwaambie Tu Huyu Kijana Ni ndugu yetu anaroho ya kipekee Tokea nimekuwa nae karibu na Kuna Makubwa kwa Bara na Visiwani kwetu Get ready msirubuniwe Njooni nilipo Nasema CHECHEI kila Mmoja aitikie CHECHEI Tusonge mbele🙏🙏 "

Ikumbukwe ATMFALME ana ngoma na ANJELLA iitwayo "Si saizi yako" ambayo imesimamiwa na kutolewa chini ya KONDEGANG.

No comments