AMKA NA BWANA LEO 21
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumatano, 21/07/2021.
*HEBU NURU YAKO NA IANGAZE.*
*Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Matendo ya Mitume 1:8.*
▶️Moyo wangu ulifurahi kuona miongoni mwa waongofu [huko Wills, Michigan] vijana wengi na wa kike na wa kiume, wakiwa na mioyo iliyolainishwa na kutiishwa na upendo wa Yesu, wakikiri kazi nzuri iliyofanywa na Mungu kwa ajili ya roho zao. Kwa kweli kilikuwa ni kipindi cha thamani hasa. "Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu." (Warumi 10:10)....
▶️Ni muhimu kwamba hawa ambao wamekuja hivi karibuni kwenye imani wawe na utambuzi wa wajibu wao kwa Mungu, ambaye amewaita wapate kuujua ukweli, na kujaza mioyo yao na amani Yake takatifu, ili waweze kuwa na mvuto utakasao juu ya wote ambao wanashirikiana nao. "Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana" (Isaya 43:10). Kwa kila mmoja Mungu amemkabidhi kazi, kuutambulisha wokovu wake kwa ulimwengu.
▶️Katika dini ya kweli hakuna kitu cha ubinafsi au cha mtu peke yake. Injili ya Kristo ni ya kutawanyika na yenye kutaka kuenea. Inaelezewa kama chumvi ya dunia, chachu inayobadilisha, nuru inayoangaza gizani. Haiwezekani mtu kupata fadhila na upendo wa Mungu, na kufurahia ushirika pamoja naye, na bado asihisi wajibu kwa ajili ya roho ambazo Kristo alizifia, ambazo ziko katika makosa na giza, zikaangamia katika dhambi zao. Ikiwa wale wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo. Laana ya kutojali itakuwa juu yao, uvivu wa roho kama wa kufa, ambao utawafanya kuwa miili ya mauti badala ya wawakilishi hai wa Yesu.
▶️ *Kila mtu lazima ainue msalaba, na kwa staha, upole, na unyenyekevu wa akili, achukue wajibu wa aliopewa na Mungu, akijishughulisha kwa juhudi binafsi kwa ajili ya wale walio karibu naye ambao wanahitaji msaada na nuru. Wote wanokubali majukumu haya watakuwa na uzoefu mbalimbali mwingi, mioyo yao wenyewe ikiwaka kwa bidii, nao wataimarishwa na kuhamasishwa katika juhudi mpya, za kudumu za kufanyia kazi wokovu wao wenyewe kwa hofu na kutetemeka, kwa sababu ni Mungu atendaye kazi ndani yao kunia na kutenda mapenzi Yake mema.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
Post a Comment