ALIETEGA BOMU KUMUUA LIONEL MESSI MBARONI

Leo Jumanne, Julai 13, kulikuwa na tishio la bomu katika uwanja wa ndege wa Fisherton huko Rosario, Argentina, kulingana na Doble Amarilla. 

Ndege ya Lionel Messi ilipangwa kuondoka kutoka uwanja huo wakati kijana huyo mwenye umri wa miaka 34 alipokuwa akiondoka kwenda likizo.

Kwa sasa, hakujakuwa na ripoti yoyote ikiwa bomu lilikuwa limewekwa ndani au nje.

Ata hivyo, mtu aliyetega Bomu hilo katika uwanja wa Rosario Airport Argentina wakati Messi na Familia yake walipokuwa wanasafiri kwenda hispania, tayari amekamatwa, na yuko chini ya ulinzi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mpaka sasa haijarukana wazi nani aliyekuwa amemtuma.

(Via; TYS SPORTS)

No comments