Advertisement

Responsive Advertisement

YANGA WAMSIMAMISHA METACHA MNATA

Uongozi wa klabu ya Yanga umesikitishwa na kitendo kisicho cha kiungwana na kimichezo kilichofanywa na mchezaji wake Metacha Mnata kwa mashabiki wetu baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting uliofanyika Jana  katika uwanja wa Benjamini Mkapa kumalizika.

Kwa kitendo alichoonyesha mchezaji, Uongozi wa Yanga unamsimamisha mchezaji Metacha Mnata kuanzia sasa hadi hapo suala lake litakapofikishwa mbele ya kamati ya nidhamu na kujadiliwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Klabu.

Uongozi unaomba radhi kwa Wanachama, Wapenzi, Mashabiki na Wadau wote wa michezo kwa ujumla kwa kitendo hicho, Uongozi utachukua hatua ya kumpeleka kwenye kamati ya Nidhamu ya Klabu kwa hatua zaidi. 

Aidha Uongozi unawaomba Wanachama, Wapenzi, Mashabiki na wadau wote wa soka kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho Uongozi unalifanyia kazi suala hili kwa mujibu wa taratibu za Klabu.

(Via;@yangasc)

Post a Comment

0 Comments