Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wametoa elimu ya masuala ya kiutumishi kwa Waheshimiwa Madiwani na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Rufiji kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Akizungumzia ujio wa Waheshimiwa Madiwani na Viongozi hao wa CCM, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. @mohamedmchengerwa amesema kwa kuwa viongozi hao ni wasimamizi wa haki za watumishi na wananchi ni vizuri wakayaelewa vema majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kuhimiza uwajibikaji na kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Serikali katika maeneo yao ya utawala.
“Nina imani mkitoka hapa mtakuwa ni chachu ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kutoka kwa Watumishi wa Umma kwani Serikali imewaajiri kwa ajili ya kuwahudumia wananchi,” Mhe. Mchengerwa alisisitiza.
Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imechukua hatua mbalimbali katika kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma, hivyo amewaomba viongozi hao ambao ni wasimamizi wa haki za watumishi na wananchi katika maeneo yao, wawahimize watumishi kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi kama ambavyo *Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan* amekuwa akisisitiza mara kwa mara.
“Dhamira ya Mhe. Rais ni kuhakikisha haki za msingi za Watumishi wa Umma zinatekelezwa ili kuwajengea ari ya kutoa huduma bora kwa umma,” Mhe. Mchengerwa ameongeza.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. @dndejembiametoa rai kwa viongozi hao kutumia elimu waliyoipata kuhamasisha watumishi kutoa huduma bora kwa wananchi.
Naye Katibu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Wilaya ya Rufiji, Comrade. Hassan Makoba amesema, wakiwa wasimamizi wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2020 watawahamasisha Watumishi wa Umma kutimiza wajibu wao ili wananchi wapate huduma bora
0 Comments