WATU MILIONI 26 KUCHANJWA NCHINI KENYA
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mipango ya kuchanja watu wote wazima wa Kenya watu milioni 26 ifikapo katikati ya mwaka wa 2022 huku milioni 10 wakiwa wamepangwa kupewa chanjo ifikapo Desemba mwaka huu.
Rais anasema mpango huu ni tofauti na ule ambao serikali ilikuwa nao mwanzoni mwa mwaka kutokana na ununuzi wa dozi milioni 13 za chanjo ya Johnson na Johnson inayowasili mnamo Agosti.
"Mkakati wetu ulikuwa kuchanja watu wazima milioni 10 ifikapo Juni 2022 na takriban milioni 16 ifikapo Juni 2023," ---Kenyatta
"Badala ya kuwachanja watu wazima milioni 10 ifikapo Juni 2022, tutachanja watu wazima wote wa Wakenya milioni 26 ifikapo mwaka 2022. Kwa kweli, kufikia Krismasi mwaka huu, tunakusudia kuwa tumewapa chanjo watu wazima zaidi ya milioni 10."---- Kenyatta
Post a Comment