Advertisement

Responsive Advertisement

WATU 13 WAUAWA SYRIA

Watu wasiopungua 13 wameuliwa na zaidi ya watu 27 walipata majeraha katika shambulio la hospitali katika mji wa Afrin Nchini Syria Jumamosi.

Kulingana na shirika la Habari la Anadolu, shambulio la hospitali ya kibinafsi lilitekelezwa na Chama cha Wafanyakazi cha Kurdistan na Vikosi vya Kujilinda vya Kikurdi vya Syria (PKK / YPG).

Katika muongo mmoja uliopita, hospitali kote Nchini Syria zimeshambuliwa zaidi ya mara 400.

Takwimu zilizopatikana na DW zinaonyesha kuwa mashambulio hayo yalikuwa sehemu ya mkakati mkubwa wa kulemaza ufikiaji wa vituo vya matibabu katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi.

Post a Comment

0 Comments