WANAOZUIA WAFANYAKAZI KUJIUNGA HATUA KUCHUKULIWA
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Watu Wenye Ulemavu Mheshimiwa Ummy Nderiananga amewaagiza waajiri nchini kuhakikisha wanawaruhusu wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi wanavyoviridhia.
Nderiananga ametoa kauli hiyo leo Juni 05, 2021 mkoani Morogoro wakati akifungua semina ya wajumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO).
Amesema serikali itachukua hatua stahiki dhidi ya waajiri wanaowazuia wafanyakazi wao kujiunga na vyama vya wafanyakazi.
“Nawaagiza tena waajiri wote kuhakikisha wafanyakazi wanajiunga na vyama vya wafanyakazi kwani ni haki yao ya msingi. Hatua stahiki zitachukuliwa kwa waajiri wanaozuia wafanyakazi kujiunga na vyama wavipendavyo,” amesema Mhe. Nderiananga
Nderiananga amesema serikali imedhamiria kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya wafanyakazi nchini na hivi karibuni serikali ilianzisha kliniki ya kazi kushughulikia migogoro kwa muda mfupi ili muda mwingi utumike katika uzalishaji.
“Kupitia wizara yetu, Ofisi ya Waziri Mkuu imedhamiria kuhakikisha migogoro sehemu za kazi kwa sehemu kubwa inapungua na kuhakikisha sheria zinazowekwa zinatekelezwa na kwamba vyama vinatekeleza majukumu yake kwa weledi na tija,” ameongeza Nderiananga.
Mbali na kufurahishwa na jitihada za TUICO katika kufunga mikataba ya hali bora za kazi hapa nchini, Naibu Waziri Nderiananga amekipongeza TUICO kwa usimamizi mzuri na uundaji wa mabaraza ya wafanyakazi, utoaji wa mafunzo na utetezi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TUICO Taifa Ndg. Paul Sangeze amesema kuna waajiri ambao hawatoi ushirikiano maeneo ya kazi hali inayochangia kukuza migogoro baina ya wafanyakazi na waajiri na hivyo kupunguza tija sehemu za kazi” amebainisha Ndg. Sangeze.
Ameiomba serikali kuhakikisha inatembelea maeneo ya kazi hasa yenye matatizo mengi ili kukuza tija, haki, heshima na maslahi ya wafanyakazi mahala pa kazi.
“Kwa hali ilivyo Dangote Cement mjini Mtwara, inapaswa kuangaliwa kwa jicho la tatu. Wafanyakazi wa kiwanda hiki wana changamoto nyingi na wameomba upatapo nafasi uwatembe

Post a Comment