Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika miradi mikubwa ya kimkakati
inayotekelezwa na Serikali.
Mhe. Rais Samia amesema hayo leo tarehe 13, Juni 2021 Jijini Mwanza wakati akizungumza na Vijana wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani wakiwawakilisha vijana nchini.
Ametaja baadhi ya miradi hiyo ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali kuwa ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa daraja la Magufuli GPM Bridge) katika eneo la Kigongo - Busisi, ujenzi wa Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere
katika mto Rufiji, Reli ya kisasa yaani SGR na ujenzi ukarabati wa Viwanja vya ndege.
Mhe. Rais amesema mbali na fursa hizo za miradi ya kimkakati pia vijana hawana budi kutumia fursa zilizopo kwenye kilimo na mifugo ambapo Tanzania ni ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo Barani Afrika.
Aidha, Mhe. Rais Samia amewataka vijana kutumia fursa za uchumi mtandao, ambapo Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye Mkongo wa Taifa na Kituo cha taifa cha kuhifadhi kumbukumbu (Data Cente. Mhe. Rais amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuanza kufikiria kujenga shule za michezo Sports Academy) katika mikoa na kujenga kumbi za kisasa za burudani na michezo Sports Arena) ambazo wasanii watazitumia katika majira yote ya mwaka.
Pia ameuagiza uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha inavikarabati viwanja vyake vya michezo ili kuwa na hadhi ya kisasa kwa ajili ya michezo Katika hatua nyingine, Mhe. Rais amezindua Chelezo ambacho kimekamilika
kujengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 36.4.
Chelezo hicho kwa sasa kinatumika kutengeneza Meli mpya ya Mv. Mwanza pia kitatumika kutengeneza na kukarabati Meli nyingine hapa nchini na hata kutoka nje ya nchi.
Mhe. Rais Samia pia amezindua Meli mbili za New Butiama na New Victoria ambazo zimefanya ukarabati mkubwa na kwasasa zinatoa huduma kama awali kwa kusafiri kati ya Mwanza na Bukoba na Nansio Ukerewe.
Katika siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Mwanza, Mhe. Rais pia ameshuhudia titiaji saini wa Mikataba mitano ya ujenzi na ukarabati wa Meli ambazo baadhi yake zitatumika kutoa huduma katika Za Tanganyika na bahari sa Hindi,
zitakazogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 438.
Mhe. Rais amemaliza ziara yake ya siku 3 mkoani Mwanza na kurejea Jijini Dar es Salaam.
0 Comments