Advertisement

Responsive Advertisement

RONALDO AWEKA REKODI LEO

Magoli mawili aliyofungia Ureno leo kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Hungary, yanamfanya 'Mwamba', Cristiano Ronaldo kuweka rekodi mpya nne kama ifuatavyo:-

1. Amekuwa ndiye mfungaji bora wa muda wote kwenye michuano ya Euro, akifikisha mabao 11.

2. Amekuwa ndiye mfungaji bora wa muda wote kwenye timu yake ya taifa ya Ureno akifikisha mabao 106.

3. Amekuwa mchezaji wa kwanza kucheza michuano hiyo mara tano mfululizo.

4. Ronaldo amekuwa ndiye mchezaji wa kwanza kufunga goli katika fainali tano mfululizo za michuano ya Euro.


NB; Portugal leo dhidi ya Hungary, wameondoka Half Time wakiwa bila bila, dakika ya 84' Raphael Guerreiro anaitanguliza Portugal  DAKIKA ya 87' Cristiano Ronaldo kupitia mkwaju wa Penalty anapachika bao, DAKIKA YA 90 zikiwa zimeongezwa dakika 5, ya 92 tu anapachika bao jingine, na kuufanya mchezo kumalizika 0 - 3.

#RESPECTRONALDO

Post a Comment

0 Comments