Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 15 Juni, 2021 ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bw. Bakari Msulwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya hiyo Bi Sheilla Lukuba kwa kushindwa kusimamia Wafanyabiashara wadogowadogo Wamachinga Mkoani Morogoro.
Mhe. Rais Samia ametangaza hatua hiyo wakati akihutubia vijana wa Mkoa wa Mwanza na Mikoa jirani waliotawakilisha vijana wote nchini.
Amesema amesikitishwa na kitendo cha Askar Mgambo katika eneo la Kituo cha Mabasi Morogoro kuwanyanyasa Wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga wanaofanya biashara nje ya Kituo
hicho.
Mhe. Rais amesema kitendo cha kunyanyasa wafanyabiashara hao si cha kiungwana na hakikubaliki kamwe.
0 Comments