SHAMBA LA VALESKA KUFUTWA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametangaza kufutwa kwa shamba la Valeska lenye ukubwa wa ekari 4,087 katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani Arusha.
Lukuvi alitangaza uamuzi huo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kufuta shamba hilo kufuatia kuombwa kufanya hivyo na Waziri wa Ardhi. Hata hivyo, Waziri Lukuvi alisema halmashauri ya wilaya ya Meru itawajibika kulipa fidia katika maeneo yanayohitaji fidia ambapo kwa mara ya mwisho fidia ilikuwa milioni 394.10.
Waziri Lukuvi alianisha matumizi ya shamba lililofutwa kuwa ni ekari 1500 kugawiwa kwa vijiji vitatu vya Kwaugoro, Valeska na Maloloni na kuongeza kuwa ekari 1028 zitatumika kwa shughuli za kilimo na ekari 1559 kwa matumizi mbalimbali kama makazi na biashara.

Post a Comment