KITUO KIPYA KURAHISISHA UPATIKANAJI HUDUMA
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo amesema kituo kipya cha huduma kwa wateja kilichoanzishwa na Wizara ya Ardhi kitarahisisha upatikanaji huduma na kuondoa urasimu katika sekta ya ardhi nchini.
Bi. Makondo alitoa kauli hiyo tarehe 1 Juni 2021 jijini Dodoma wakati akimtembeza katika jengo la Wizara ya Ardhi na kituo kipya cha Huduma kwa Wateja Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Prof. Godius W. Kahyarara katika Mji wa Serikali uliopo eneo la Mtumba.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, moja ya malengo ya kuanzishwa kituo hicho cha huduma kwa wateja ambacho kiko katika hatua za mwisho kukamilika ni kuwahamasisha wawekezaji kwa kurahisishia upatikanaji huduma na kuondoa urasimu alioueleza kuwa kero kubwa kwa wawekezaji wengi.
Akielezea jinsi kituo hicho kitakavyoweza kuwasaidia wawekezaji, Bi. Makondo alisema moja kati ya madawati yatakayowekwa kwenye kituo hicho ni Umilikishaji ardhi na masuala ya kodi ya pango la ardhi ambapo mwekezaji hatahitaji kufuata huduma ofisini bali atapiga simu kokote alipo na suala lake kuelekezwa sehemu husika na kutatuliwa.
Aidha, katika kuongeza ufanisi, Bi. Makondo alifafanua kuwa, mifumo iliyowekwa ndani ya kituo hicho itakuwa ikitoa muda maalum wa ombi lililosajiliwa kushughulikiwa na ikitokea muda uliowekwa umepita bila kushughulikiwa basi ombi husika litapelekwa hatua nyingine ya juu ili liweze kutatuliwa.
Kwa Mujibu wa Makondo, hatua hiyo itaondoa ile hali ya ucheleweshaji huduma katika sekta ya ardhi.
Akielezea zaidi kuhusu uendeshwaji wa kituo hicho cha Huduma kwa Wateja, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Wizara ya Ardhi Bw. Venance Mworo alisema kuwa, kwa sasa mafunzo yameanza kutolewa kwa watumishi watakaohusika moja kwa moja kutoa huduma hizo na kubainisha kwamba. kila kitu kinachohitajika kwenye kituo kimeshakamilika.

Post a Comment